BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Dazlah Kurudiana Na Liz Jahsoljia.

Mwaka wa 2017 haujakua wa nuru sana kwa msanii Dazlah Kiduche mkali wa Kide kide licha yakuachilia kazi kadhaa mwaka huu ikiwemo Amamadodo, Waongee na nyenginezo ngoma ambazo hazikupokelewa vyema na mashabiki wake  wamekua wakidai msanii huyo anafaa kutafakari tena na kutoa goma kali kama Kide Kide ambayo ilitawala sana airwaves.

Hayo yakiwa tisa kumi ni wengine wanahoji kuwa tangu msanii huyo aachane na mpenzi wake wa zamani Liz Jahsoljia hali imekua ngumu kwa msanii huyo kwani ameshindwa kutamba kwenye tasnia hiyo mwaka huu.

Awali wawili hao walikua wapenzi waliopigiwa mfano katika ulingo wa burudani na wengi walitamani penzi lao liendelee lakini liliingiliwa na shetani na hatimaye likafika kikomo ghafla.

Lakini sasa kuna tetesi mitaani kuwa wawili hao wanamatamanio yakurudiana na mdaku wetu katika meza ya soga za usanii anatudokeza kwamba wawili hao wanawasiliana chini ya maji kulirudisha penzi lao lilomea nyasi.

Dazlah ambaye anatarajiwa kuachilia ngoma yake mpya wiki hii anadaiwa kuitunga nyimbo hio mahususi kumbembeleza Liz arudi kwenye ulingo wake.

Meneja wa Dazlah ambaye pia ni produza wake Mr Tee amenukuliwa akisema litakua ni jambo la busara kama hilo litatokea ila anasema chamsingi kwake yeye ni kuhakikisha msanii wake anapata mafanikio mwaka wa 2018 na kuwa mmoja wa wasanii wakubwa katika taifa la Kenya.

Kwenye siku za hivi karibuni Liz amekua kimia sana kwenye mitandao na kuna madai wawili hao wanamawasiliano ya kisiri.

Haya habari ndio hio sisi letu nijicho tu na tunaifatilia habari hii ikiiva meza ya soga za usanii tutakupakulia.

 

 

Show More

Related Articles