HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaharakati Wa Shinikiza Dori Atiwe Mbaroni

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu chini ya mwamvuli wa Kwale active  citizen for peace wanaitaka idara ya usalama kumkamata mbunge wa Msambweni Suleimani Dori  kwa kile wanachokitaja  kuwa anachochea wananchi dhidi ya wawekezaji hususan yule wa kampuni ya uchimbaji madini ya Base titanium.

Mwanzilishi wa shirika hilo la kijamiii Juma Mwasifa akishinikiza vyombo vya usalama kumchukulia hatua za kisheria mbunge huyo akisema kuwa analenga kuhujumu amani eneo la Msambweni .

Haya yanajiri baada ya Dori  kunukuliwa kuongoza maandamano dhidi ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya base titanium kwa madai ya kudhulumu Wananchi.

Hata hivyo  inakisiwa kuwa kelele za  dori  zimetokana na yeye kupokonywa kandarasi aliyokua amepewa na kampuni ya base.

Show More

Related Articles