HabariPeople DailyPilipili FmPilipili FM News

Wandayi Achaguliwa Kama Mwenyekiti Wa Kamati Ya Hesabu Bungeni

Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi amechaguliwa kama mwenyekiti wa kamati ya hesabu za umma bungeni.

Wandayi ambaye anahudumu katika muhula wake wa pili alipata kura 15 kati ya wabunge 18 waliopiga kura, na kumshinda mpinzani wake mkuu Sakwa Bunyasi aliyepata kura 3 pekee.

Wandayi ambaye anajulikana kwa kuwa na matamshi makali dhidi ya chama tawala cha jubilee, amesema atatekeleza majukumu yake bila uoga wala upendeleo.

Mbunge wa Kibwezi Jessica Mbalu amechaguliwa naibu mwenyekiti wa kamati hiyo, na kuwaomba wajumbe wa kamati hiyo kudumisha umoja kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

Naye mbunge wa Kajiado Kusini Katoo Ole Metito amechanguliwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi bungeni.

Show More

Related Articles