HabariPilipili FmPilipili FM News

Viongozi Wa Kidini Wa Kashifu Shinikizo la Kumwapisha Raila

Viongozi wa kidini Kaunti ya Kilifi wamekashifu vikali hatua ya baadhi ya viongozi wa pwani kuendelea kushinikiza kuapishwa kwa kinara wa NASA Raila Odinga kuwa rais wa mabunge ya wananchi.

Viongozi hao akiwemo kiongozi wa kanisa la kiangilikana eneo hilo Askofu Lawrence Dena amesema hatua hiyo iko kinyume cha sheria na kwamba inalenga kuwahadaa wananchi, akiongeza kuwa taifa la Kenya haliwezi kuwa na marais wawili.

Amewataka viongozi kuhubiri amani na kuunganisha wananchi bila kuweka uchochezi na ubaguzi

Show More

Related Articles