HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mwanasheria Mkuu aonya mashtaka ya uhaini yatamkabili Raila akijiapisha

Mwanasheria Mkuu wa serikali Prof Githu Muigai ameshikilia msimamo wa kuwa kitendo cha kumuapisha kinara wa upinzani NASA Raila Odinga kitatambulika kama kitendo cha uhaini yaani treason na hivyo basi atachukuliwa hatua kali za kisheria iwapo hilo litatimia.

Msimamo wa Prof Muigai kama mshauri mkuu wa serikali unawadia wakati juhudi za upatanisho wa mazungumzo zinapozidi kugonga mwamba huku NASA ikidai kuwa ifikiapo mwishoni mwa mwaka huu, basi Raila Odinga ataapishwa.

Show More

Related Articles