HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya Thika jana yafikia 22

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali mbaya katika barabara ya Thika kuelekea Garissa maeneo ya kilimambogo imefikia 22 baada ya majeruhi waliokimbizwa hospitalini kufariki.
Watu sita pia wamejeruhiwa vibaya kwenye ajali nyingine maeneo ya Molo katika barabara ya Nakuru kuelekea Eldoret ambapo dereva wa gari la shule alikosa mwelekeo na gari kuanguka kwenye mtaro huku akijaribu kukwepa kugongana na gari lingine lililokuwa linaendeshwa kiholela.
Visa hivi vya ajali mwezi wa disemba vimeonekana kuongezeka huku washikadau wakilaumiana kuhusu utepetevu wa madereva barabarani.

Show More

Related Articles