HabariMilele FmSwahili

Judy Wakhungu azindua mradi wa kuhifadhi chemichemi za maji

Waziri wa mazingira na mali asili Judy Wakhungu amezindua mradi wa  kuhifadhi chemichemi za maji utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.Wakhungu anasema mradi huo  wa kulinda vyanzo na chemichemi za maji utawafaidi wenyeji wa Magharibi mwa nchi na Bonde La Ufa.Akiongea wakati wa hafla hiyo gavana wa Elgeyo Marakwet Alex Tolgos amepongeza hatua ya serikali kutengea kila kaunti shilingi milioni 16 kufanikisha mpango huo.

Show More

Related Articles