HabariMilele FmSwahili

Serikali yapanga kuendesha hesabu ya kitaifa ya watoto wa mitaani

Serikali inapanga kuendesha hesabu ya kitaifa ya watoto wa mitaani ili kubaini idadi yao.Zoezi hilo litakaloandaliwa kuanzia mwezi Januari litaifanya Kenya kuwa taifa la kwanza Afrika Mashariki na Kati kubaini hesabu ya watoto hao.Shughuli hiyo itakayoendeshwa na wizara ya mipango kwa ushirikiano na shirika la kitaifa la hesabu itagharimu shilingi milioni 50.Mkurugenzi wa hazina ya kurekebisha tabia ya watoto hao Robert Njogu anasema imekuwa vigumu kutekeleza mipango yao kwa kukosa takwimu kamili za watoto hao.

Show More

Related Articles