HabariMilele FmSwahili

Mahakama yaagiza Kenya Airways kurejesha wahandisi na mafundi 157 waliofutwa kazi

Shirika la ndege Kenya Airways limeagizwa kuwarejesha kazini mara moja wahandisi na mafundi 157 wake waliofutwa kazi baada ya kugoma. Jaji wa mahakama ya viwanda Helen Wasilwa ameagiza wafanyikazi hao kurejea kazini hadi kesi waliyowasilisha kupinga kufutwa kazi iamuliwe. Wafanyikazi hao walifutwa kazi baada ya kugoma mwezi uliopita kushinikiza nyongeza ya mishara yao.

Show More

Related Articles