MichezoMilele FmSwahili

Kiungo wa kati wa zamani wa AC Milan na Real Madrid Kaka astaafu soka

Kiungo wa kati wa zamani wa AC Milan na Real Madrid Kaka ametangaza kustaafu soka.Kaka alishinda Kombe la Dunia mwaka 2002 akiwa an Brazil.Mchezaji huyo wa miaka 35 alianza uchezaji soka wake Brazil akiwa na klabu ya Sao Paulo, na amekuwa akichezea Orlando City inayocheza Ligi Kuu ya Amerika ya Kaskazini (MLS).

Kaka alicheza mechi yake ya mwisho Oktoba Orlando walipomaliza msimu, na mwezi Novemba taarifa zilisema alikuwa amepewa kazi ya kuwa mkurugenzi katika klabu ya AC Milan.Yeye ni miongoni mwa wachezaji wanane pekee waliowahi kushinda Kombe la Dunia, Kombe la Ulaya/Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na tuzo ya Ballon d’Or.

Wengine ni Bobby Charlton, Gerd Muller, Franz Beckenbauer, Paolo Rossi, Zinedine Zidane, Rivaldo na Ronaldinho.Kaka alichezea Brazil mechi 92 na kuwafungia mabao 29.Baada ya kushinda Kombe la Dunia, alishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Milan mwaka 2007 na akakabidhiwa tuzo ya Ballon d’Or (tuzo ya mchezaji bora duniani) mwaka huo.

Show More

Related Articles