HabariMilele FmSwahili

Mabunge ya kaunti yatakiwa kujitenga na shinikizo la NASA kubuni mabunge ya halaiki

Mabunge ya kaunti yametakiwa kujitenga na shinikizo za NASA za kubuni mabunge ya halaiki. Mbunge wa Soy Caleb Kositany amewataka wawakilishi wadi kukomesha mijadala kuhusu hoja ya kubuni mabunge hayo na kuzingatia maswala ya maendeleo. Kositany pia amemtaka kinara wa NASA Raila Odinga kukomesha harakati zake za kuapishwa na kushirikiana na rais Uhuru Kenyatta kuwatumikia wananchi. Amesema hatua ya wabunge wa Jubilee kumuunga mkono Dkt Oburu Oginga na Kennedy Musyoka kuwa wabunge katika bunge la Afrika Mashariki ni ishara kuwa serikali iko tayari kufanya kazi na upinzani ili kuunganisha taifa baada ya uchaguzi.

Show More

Related Articles