HabariMilele FmSwahili

Ukabila na siasa zaadhiri zaidi usimamizi wa vyuo vikuu nchini

Ukabila na muingilio wa kisiasa umetajwa kuathiri zaidi usimamizi wa vyuo vikuu nchini. Akiongea katika mkutano wa wajumbe wa chama cha UASU mwenyekiti wake Muga Kolale anasema masuala hayo yameingizwa katika shughuli ya kutoa nafasi za ajira na kupandishwa vyeo kwa wafanyikazi na hivyo kuathiri viwango vya huduma zinazotolewa. Anasema kuna baadhi ya vyuo ambavyo vimekosa kuwapandisha vyeo wafanyikazi wake kwa muda kwa kuwa wafanyikazi waliohitimu kupewa nafasi hizo si wenyeji wa jamii hizo.

Show More

Related Articles