HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa Wa Uwindaji Haramu Watiwa Mbaroni Kwale

Washukiwa 3  wa uwindaji haramu wamekamatwa na maafisa wa shirika la uhifadhi wa wanyamapori  kaunti ya kwale  wakiwa na bidhaa za wanyamapori zenye thamani ya shilingi  5M katika maeneo tofauti ya kaunti hiyo.

Saidi Kuzidi Mwachitema  ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi ya mwamasa huko kinango amekamatwa eneo la Mtsangatamu huko matuga akiwa na pembe 2  za ndovu  zenye uzani wa kilo 34  huku Hasira Makotti Mwanzalla aliyemfanyikazi wa serikali ya kaunti ya kwale amepatikana pembe   2  za ndovu  zenye uzani wa kilo 16  kutoka eneo la Tiribe huku Wambua Kilanze akipatikana na ngozi mbili za chui eneo la meli nane huko kinango .

Afisaa wa shirika hilo Nathan Gatundu aliyekua akizungumza na wanahabari afisini mwake amesema kuwa wamepata habari za washukiwa hao kutuka kwa wananchi

 

Show More

Related Articles