HabariSwahiliVideos

Wabunge 9 wa Kenya hatimaye kuapishwa Arusha,Jumatatu

Wabunge tisa waliochaguliwa kuwakilisha Kenya katika bunge la Afrika mashariki wanatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatatu mjini Arusha Tanzania, tayari kwa vikao vya bunge hilo Januari mwakani.
Tisa hao wanaojumuisha watano kutoka mrengo wa Jubilee na wanne kutoka NASA, waliponea kwenye kinyang’anyiro cha kufa kupona bungeni ambacho kiliendelea hadi saa sita usiku hapo jana.
Kama anavyotuarifu Kiama Kariuki, kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka anatarajiwa kurejea hapa nchini kesho kutoka Ujerumani, ili kuhudhuria kuapishwa kwa mwanawe Kennedy Musyoka, ambaye alichaguliwa kwa kura nyingi zaidi.

Show More

Related Articles