HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahudumu Wa Tuktuk Kupokea Mafunzo Kuanzia Mwaka Ujao

Chama cha ushirika   cha wahudumu wa tuktuk kaunti ya Mombasa wakishirikiana na kampuni ya safaricom wameanzisha mazungumzo ili madereva wa tuktuk wapewe Till Number ya kupokea malipo yao kutoka kwa wateja.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa sacco hiyo Benson Njoroge amesema wahudumu wa tuktuk wanahitaji till namba hiyo kwa sababu ya uhuni unaondelezwa na baadhi ya wateja wanaowabeba.
Hii ni baada ya baadhi ya madereva wa tuktuk kulalamika kuporwa pesa zao na baadhi ya wateja wanaowabeba.

Wakati huo huo Njoroge amesema watatoa mafunzo kwa wahudumu wa tuktuk kuanzia mwaka ujao kwa ada kidogo ili wapate leseni na ujuzi bora wa kuendesha tuktuk zao.
Naye naibu kamishna kaunti ya Mombasa Mohammed Maalim amewataka madereva hao kuwa na nidhamu haswa msimu huu wa likizo ikizingatiwa kuwa kuna wageni wengi mjini.

Show More

Related Articles