HabariMilele FmSwahili

Magavana kumchagua mwenyekiti mpya na naibu wake leo

Magavana watamchagua mwenyekiti mpya na naibu wake leo bila kuegemea misimamo ya kisiasa. Kulingana na gavana wa Bomet Joyce Laboso magavana wa Jubilee hawajashurutishwa na rais Uhuru Kenyatta kumchagua mgombea yeyote licha ya chama hicho kumuunga mkono gavana wa kwale Salim Mvurya kuwa mwenyekiti mpya. Amesema baraza la magavana limeweka mikakati kuwachagua viongozi wenye tajriba na uwezo wa kuendesha ajenda ya maendeleo katika kaunti. Uchaguzi wa viongozi wapya wa baraza la magavana utafanyika leo katika mkutano wa magavana unaoendelea kaunti ya Kwale. Wakati huo huo gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki amewasuta baadhi ya magavana waliosusia mkutano huu akionya hatua hiyo inahujumu juhudi za kuhimiza ushikamano nchini.

Show More

Related Articles