HabariMilele FmSwahili

Oburu Odinga na Kennedy Musyoka ni miongoni ya waliochaguliwa katika bunge la EALA

Nduguye kinara wa NASA Oburu Odinga na mwanae Kalonzo Musyoka Kennedy Musyoka ni miongoni mwa waliochaguliwa kuiwakilisha Kenya  katika bunge la afrika mashariki EALA. Musyoka alipigiwa kura 309 huku Oburu akipata kura 243 naye Abdikadir Aden aliyepata kura 234 na Fatuma aliyeungwa mkono na wabunge (143) wakikamilisha orodha ya wawakilishi wanne wa muungano wa NASA. Kutoka upande wa Jubilee wawakilishi watano waliochaguliwa ni mbunge wa zamani wa kamukunji Simon Mbugua aliyepata kura 286 Florence Jematia (252), Mpuru Aburi (208), Wanjiku Muhia (180), na  Adan Noor (192). Wawakilishi hao sasa wataapishwa rasmi katika bunge la EALA jijini Arusha Tanzania Jumatatu ijayo.

Show More

Related Articles