HabariK24 TvSwahiliVideos

Mahakama ya Upeo yaharamisha hukumu ya lazima ya kifo

Mahakama ya upeo katika uamuzi wa kipekee humu nchini, imetupilia mbali hukumu ya kifo cha lazima kwa kunyongwa, na kusema kwamba ni kinyume cha sheria na kwamba haiambatani na katiba mpya.
Hayo yaliafikiwa baada ya wafungwa wawili, waliohukumiwa kifo mwaka wa 2003,  Francis Murwatetu na Wilson Thrombus kuitaka mahakama ya juu zaidi nchini kuelezea kwa kina hukumu ya kifo.
Majaji Philomena Mwilu,Jackton Ojwang’ na Njoki Ndung’u  aidha walisema kwamba huenda hukumu hiyo ikakandamiza haki za kibinadamu za wafungwa.

Show More

Related Articles