HabariMilele FmSwahili

Hukumu ya kifo ni kinyume cha katiba ya Kenya

Hukumu ya kifo ni kinyume cha katiba ya humu nchini. Ndio uamuzi wa jopo la majaji 6 wa mahakama ya juu zaidi waliokuwa wanashughulikai kesi iliyowasilishwa na wafungwa wawili waliotaka hukumu hiyo kuondolewa. Majaji hao wanasema hukumu hiyo imekiuka haki hasaa ya maisha hivyo wakaiharamisha. Wafungwa Francis Karioko na Wilson Thirimbu wawalikuwa wamewasilisha kesi katika mahakama ya juu baada ya ile ya rufaa kuwahukumiwa kifo kutokana na mauaji waliyotekeleza miaka 16 iliyopita. Wawili hao walidai uamuzi huo umewadhalilisha na kukiuka haki yao ya kuishi

Show More

Related Articles