HabariMilele FmSwahili

Kongamano la 60 la wajumbe wa KNUT kuandaliwa leo mjini Mombasa

Kongamano la 60 la wajumbe wa kitaifa wa chama cha walimu KNUT linaandaliwa leo mjini Mombasa. Ni mkutano unaofuatia mvutano uliokumba chama hicho kuhusiana na hatua ya kustaafishwa mwenyekiti anayeondoka Mudzo Nzili. Nzili pamoja na naibu wake Samson Kaguma wanatarajiwa kutoa hatuba yao ya kuwaaga walimu katika kongamano hilo la siku tatu. Aidha agizo la serikali kwa katibu mkuu Wilson Sossion kujiuzulu baada ya kuteuliwa mbunge linatarajiwa kujadiliwa leo.

Show More

Related Articles