HabariMilele FmSwahili

Sossion na Milemba watakiwa kung’atuka afisini mara moja

Willson Sossion wa KNUT na Omboko Milemba wa KUPPET ni baadhi ya viongozi wa miungano nchini wanaofaa kung’atuka afisini mara moja.Kwenye agizo lililochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali waziri wa leba Phillis Kandie anasema wawili hao pamoja na magavana Mutahi Kahiga wa Nyeri na Stanley Kiptais wa Baringo wanafaa kuzingatia nyadhifa zao katika siasa.Agizo hili likiwadia saa chache baada ya waziri wa elimu dr Fred Matiangi kuwataka Sossion na wenzake wanaokerwa na mabadiliko katika sekta ya elimu kufika mahakamani kupinga mabadiliko hayo.

Show More

Related Articles