HabariPilipili FmPilipili FM News

Mabalozi Wa Nyumba Kumi Wadaisha Mshahara

Mabalozi wa nyumba kumi huko msambweni kaunti ya kwale wameitaka serikali ya kitaifa kuwalipa mshahara kufuatia mchango wao mkubwa wa kuleta amani na uiano miongoni mwa jamii.

Haya ni kwa mujibu   wa Juma Nasoro ambaye ni mwenyekiti wa makundi ya nyumba kumi,  akizungumza na waandishi wa habari eneo la shimbahills .

Nasoro anasema tangu kenya ijipatie uhuru mwaka wa 1963, wazee wa nyumba  kumi pamoja na wale wa vijiji hawajawahi  pewa ruzuku kutoka  kwa serikali, licha ya wao kuchangia katika umoja wa kitaifa.

Show More

Related Articles