HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Taita Taveta Wavamiwa Na Majambazi Kutoka Nchi Jirani

Viongozi wa utawala wakiongozwa na kamishna wa kaunti ya Taita-Taveta Kula Hache wamekashifu hatua ya raia kutoka mataifa  jirani kuvamia mashamba ya wakazi wa kaunti hiyo.

Haya ni baada ya mshukiwa mmoja mwenye asli ya Kitanzania kupatikana akimiliki silaha kinyume cha sheria , na pia kuiba machimbo ya madini mjini mwatate.

Kwa sasa mshukiwa anazuiliwa na polisi huku akitarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo.

Naye Kiongozi wa wengi kwenye bunge la kaunti ya Taita Taveta Jason Tuja ametaka mzozo wa mpaka kati ya Kaunti hiyo na ile ya Kwale kutatuliwa

Show More

Related Articles