HabariMilele FmSwahili

Idadi ya waliofariki katika ajali ya Sachang’wan yafikia 30

Watu zaidi ya 30 wamedhibitishwa kufariki kufuatia ajali mbaya ya bara barani eneo la Sachang’wan bara bara ya Eldoret Nakuru. Ajali hiyo imehusisha magari 13 ikiwemo matau basi na lori ambalo dereva anadaiwa alikuwa akiwatoroka maafisa wa NTSA kabla ya kusababisha ajali hiyo. Watu wengine 28 wamejeruhiwa na wamelazwa katika hospitali mbalimbali mjini Molo na Nakuru. Juhudi za kuwaokoa abiriambao wamekwama kwa magari pia zinaendelea.

Show More

Related Articles