HabariMilele FmSwahili

Watu 10 wafariki katika ajali eneo la Sachang’wan barabara ya Eldoret Nakuru

Watu 10 wamedhibitishwa kufariki kufuatia ajali mbaya ya bara barani eneo la Sachangwan bara bara ya Eldoret Nakuru. Ajali hiyo imehusisha basi matatu kadhaa na Lori. ajali hii imetokea huku watu 19 wakidhibitishwa kufariki katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika daraja la Kamkuywa bara bara ya Kitale Webuye. 10 kati wamedhibitishwa kuwa watu wa familia moja. Kulingana na OCPD wa Bungoma kaskazini Eliud Okello matatu iliyokuwa ikisafiri kutoka Kitale kuelekea webuye iligonga tingatinga lililokuwa likisafirisha miwa. Walioshuhudia wanasema matatu hiyo iliyokuwa ilikuwa ikiendeshwa kwa kasi ilipogonga lori la kusafirisha miwa.

Show More

Related Articles