HabariMilele FmSwahili

Wafungwa mjini Kericho kujumuika na jamaa zao leo kama sehemu ya maadhimisho ya Jamuhuri

Wafungwa kwenye magereza mbalimbali mjini Kericho wameratibiwa kujumuika na jamaa zao leo kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Jamuhuri. Kamanda wa magereza kaunti hiyo William Kati anasema lengo la hafla hiyo ni kuwafahamisha wafungwa hao kuhusu jinsi ya kuishi na jamii watakapoachiliwa. Kati aidha ametoa mwito kwa jamii kuwakubali wafungwa hao pindi wanapokamilisha vifungo vyao.

Show More

Related Articles