HabariMilele FmSwahili

 Tume ya NCIC na idara ya polisi zastahili kufanyiwa Marekebisho

Tume ya uwiano NCIC pamoja na idara ya polisi zinastahili kufanyiwa marekebisho. Ndio wito wa kundi moja la kina mama linalosema kuwa taasisi hizo zilikosa kutekeleza majukumu yake vilivyo wakati wa chaguzi zilizopita. Winne Njenga mwenyekiti wa kamati kuu ya kundi hilo anasema NCIC ilionekana kuegemea upande mmoja katika kuwakabili wanaoeneza chuki. Nao polisi wamelaumiwa kwa kuhusika na visa vya uhalifu ikiwemo ubakaji wa kina mama na wasichana na kupora wakati wa ghasia badala ya kuwalinda wakenya.

Show More

Related Articles