HabariMilele FmSwahili

Kenya yaadhimisha siku ya Jamuhuri leo

Kenya inaadhimisha siku ya Jamhuri leo. Sherehe za leo zitaadhimishwa katika uwanja wa Kasarani hapa Nairobi. Msemaji wa serikali Eric Kiraithe anasema kuwa usalama umedumishwa vilivyo katika uwanja huo akiwahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi. Kilele cha sherehe hizo kitakwua ni hotuba kutoka kwa rais Uhuru Kenyatta ambaye ataweka bayana mikakati ya kuhakikisha taifa linaeendelea kusonga mbele hasa bada yake kuchukua hatamu ya uongozi kwa kipindi cha pili. Ikumbukwe kuwa Kenya ilijipatia Uhuru kutoka kwa mikono ya wakoloni tarehe 12 mwezi Desemba mwaka 1963 na maadhimisho ya Jamhuri hutumiwa kutathmini hatua zilizopigwa tangu enzi hizo.

Show More

Related Articles