HabariPilipili FmPilipili FM News

Taifa Kuidhimisha Miaka 54 Tangu Ijinyakulie Uhuru

Rais uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto leo wanatarajiwa kuongoza wakenya katika maadhimisho ya sherehe za jamuhuri katika uwanja wa kasarani jijini Nairobi.
Kulingana na msemaji wa Serikali Eric Kiraithe, milango ya uwanja huo ilipangwa kufunguliwa kuanzia majira ya saa moja asubuhi ili kuwaruhusu wananchi na wageni mashuhuri kuingia ndani ya uwanja huo.
Sherehe hizo zitang’oa nanga rasmi mwendo wa saa nne baada ya rais na naibu wake kufika katika uga wa kasarani.
Taifa la kenya linaadhimisha miaka 54 tangu lijipatie uhuru wake mwaka 1963.

Show More

Related Articles