BiasharaMilele FmSwahili

Wakulima wa ng’ombe wa maziwa kunufaika na mitambo ya kuhifadhi maziwa

Wakulima wa ng’ombe wa maziwa watanufaika na  mitambo 350 ya kuhifadhi maziwa iliyotolewa na serikali. Mkurugenzi wa kitengo cha mifugo katika wizara ya kilimo Dkt Julius Kiptarus anasema mitambo hiyo itawasaidia wakulima kupunguza hasara wanayopata bidhaa hiyo inapoharibika. Anasema mitambo hiyo iliyo na uwezo wa kuhifadhi lita 3000 ya maziwa ilinunuliwa kwa shilingi bilioni 2.2 na itasambazwa katika kaunti 9. Akiongea huko Kiambu anasema tayari mitambo hiyo imewasilishwa katika kaunti za Uasin Gishu, Nandi, Embu na Kiambu.

Show More

Related Articles