People Daily

Uvundo Mkali Waathiri shughli Za Biashara Karama

Wakaazi wa karama, kongowea  kaunti ya Mombasa wanalalamikia kuwepo kwa jaa kubwa la taka eneo hilo hali ambayo wanahofia kuwa huenda ikachangia mkurupuko wa magonjwa hatari kama vile kipindu pindu iwapo haitashughulikiwa kwa haraka.

Wakiongea na meza yetu ya habari, wengi wao wamelaumu viongozi eneo hilo kwa kuwapa ahadi nyingi za uongo kuhusu mikakati ya kushughulikia tatizo hilo, jambo ambalo kufikia sasa bado halijashughulikiwa.

Kwa upande wao wanabiashara eneo hilo wamelalamikia kuathirika kwa shughli zao pakubwa kutokana na uvundo mkali unao tokana na jaa hilo.

Show More

Related Articles