HabariMilele FmSwahili

Mwanaume aliyempiga risasi muuguzi kusalia rumande kwa wiki mbili

Mwanaume mwenye matatizo ya kiakili anayedaiwa kumpiga risasi na kumuua muuguzi katika kituo kimoja cha afya hapa jijini Nairobi atasalia rumande kwa wiki mbili.  Mahakama ya Nairobi imeagiza kuwa Joseph Mungai anayekabiliwa na kesi ya maujai azuiliwe katika gereza la Industrial area huku uchunguzi ukiendelea kuhusu hali yake ya kiakili. Mungai aliripotiwa kutekeleza mauaji hayo wiki iliyopita.

Show More

Related Articles