HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Msambweni Wapinga Mradi Wa Kuhifadhi Mazingira Ya Bahari

Wakaazi wa kijiji cha mwakamba huko msambweni  kaunti ya kwale wanaendeleza  maandamano  kupinga mradi wa kuhifadhi mazingira ya bahari eneo hilo unaolengwa kutekelezwa katika ufuo wa bahari ya umma ya kongo Beach huko diani.

Wanasema endapo mradi huo utakelezwa na shirika la hifadhi ya wanyamapori nchini KWS, utawazuia kuendesha shughuli zao za uvuvi, ambazo ndio tegemeo lao la pekee la kujipatia mapato.

Hassan Mwasipho ambaye ni mvwakilishi wa wadi eneo hilo amesema wenyeji hutegemea pakubwa  shughuli za bahari kujikimu kimaisha, na  hivyo haitakua vyema kuwaekea kikwazo kutokana na kutekeleza mradi huo.

Naye Neema Bofulo mkaazi wa kijiji cha Mwakamba amewataka wenyeji kuwa na umoja katika kuupinga mradi huo ili kuona kuwa shughuli zao hazitatizwi

Show More

Related Articles