HabariMilele FmSwahili

Majaji wa mahakama ya juu kuelezea sababu za kuidhinisha ushindi wa rais Uhuru katika uchaguzi wa Oktoba 26 leo

Majaji wa mahakama ya juu leo wanatarajiwa kuelezea kikamilifu sababu zilizopelekea kuafikia uamuzi wa kuidhinisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi wa Oktoba 26. Sheria za mahakama ya juu zinawapa majaji hao muda wa siku 21 kutoa uamuzi wake muda uliokamilika. Majaji hao kesho alasiri wataelezea kwa kina sababu za kuidhinisha kwa pamoja ushindi wa rais licha ya utata uliokuwepo. Baadhi ya masuala yanayostahili kuangaziwa kwenye maamuzi yao ni iwapo tume ya IEBC ilikosea kwa kuendesha uchaguzi wa marudio pasipo kuendesha zoezi la uteuzi na kutangaza matokeo baada ya uchaguzi kukosa kufanyika katika maeneo bunge 25.

Show More

Related Articles