HabariPilipili FmPilipili FM News

Matiangi Akashifiwa Na Muunga Wa Wafanyi Kazi Wa Vyuo Vikuu

Muungano wa wafanyikazi wa vyuo vikuu nchini ,KUSU  wamekashifu hatua ya waziri wa elimu, Fred Matiangi kuwataka wafanyikazi wa vyuo hivyo kutopewa ajira ya daima.

Akizungumza na wanahabari katika hoteli moja hapa Mombasa,Katibu  mkuu wa muungano huo, Charles Mukwaya ametaja hatua ya Matiangi  kama ya kibinafsi  na kumtaka kuwahusisha washikadau katika sekta ya elimu katika majadiliano kabla ya kufanya uamuzi.

Wakati huo huo, wafanyikazi hao wamemtaka mkuu wa chuo cha Masinde Muliro,Fredrick Otieno  kuondoka afisini kama alivyoagizwa na tume ya kupambana na ufisadi nchini, EACC  hadi uchunguzi utakapokamilika.

 

Show More

Related Articles