HabariPilipili FmPilipili FM News

Wananchi Waombwa Kutoa Ripoti Kuhusu Wahalifu

Kuna haja ya wananchi na wazee wa mitaa kujua ni jinsi gani wanavyoweza kufikisha ripoti zinazotokea mitaani kwa vyombo husika ili watu na mali zao ziweze kuwa salama.

Akiongea na wanahabari kwenye mkutano wa usalama katika lokesheni ya naibu msaidizi wa kamishna  gatuzi  la Changamwe Monica Thiong’o,amesema kuwa wanajukumu la kuwapa hamasisho wazee wa nyumba kumi vile watakavyofanya kazi.

Hiyo ni baada ya kuibuka visa mfululizo vya vijana kukaba watu na kuwaibia karibu na shule ya msingi ya Kipevu.

Thiong’o amesema kuwa ili waweze kufanya kazi yao kikamilifu ni lazima wakaazi wajitolee kuwapa ripoti badala ya kuficha wahalifu.

Show More

Related Articles