HabariPilipili FmPilipili FM News

Sekta Ya Utalii Pwani Yainuka

Sekta ya utalii ukanda wa Pwani imepigwa jeki kutokana na watalii zaidi ya lefu 8 kuzuru hoteli mbali mbali eneo la Diani kaunti ya Kwale huku zaidi ya wakaazi 300 wakipata ajira kwenye hoteli.

Watalii hao ni pamoja na wana michezo wa sky diving wanaoshiriki tamasha la Diani Beach Festival linaloandaliwa katika hoteli ya Alliance Safari kukuza utalii sawia na kubuniwa ajira kwa vijana.

Katibu wa utamaduni na vijana kaunti ya Kwale Ramadan Mugalo amesema tamasha hilo litasaidia kukuza utalii nchini.

Mkurugenzi wa tamasha hilo Sandip Patel amesema tamasha hilo limeleta pamoja zaidi ya mataifa 37 na litakamilika tarehe 10 mwezi januari.

Show More

Related Articles