HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mwanafunzi aliyedaiwa kutengeneza kilipuzi sasa adai haki 

Mapema mwaka huu mwanafunzi mmoja, Joseph Kamau wa chuo kikuu cha Multimedia aligonga vichwa vya habari baada ya kutiwa mbaroni na maafisa wa kitengo cha kukabiliana na ugaidi, A.T.P.U, kwa kudaiwa kubuni kilipuzi cha kujitengenezea na kuzua taharuki chuoni.

Licha ya barobaro huyo kupachikwa jina gaidi na baadhi ya wakenya haswa katika mitandao ya kijamii na hata kutishiwa kimaisha, Joseph aliondolewa mashtaka na kesi hiyo kutupiliwa mbali.

Mwahabari wetu Shukri Wachu alipatana na jamaa huyo na kutueleza jinsi kifaa butu kilichopaswa kutumika katika filamu ya shule kilitishia maisha yake.

Show More

Related Articles