HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Githu Muigai: Jaribio la kujiapisha ni uhaini wa hali ya juu

Mwanasheria Mkuu Profesa Githu Muigai ameitaja kama kitendo cha ukiukaji mkubwa wa sheria na uhaini, mpango wa kumwampisha kinara wa NASA Raila Odinga jumanne ijayo.

Githu amemwonya kwamba kutekeleza tishio lake ni kosa ambalo adhabu yake ni kifo akimtaka kuheshimu katiba na kukoma kuwahadaa wafuasi wake.

Aidha ameyataka mabunge ya kaunti yanayojadili hoja ya kubuni mabunge ya halaiki kujiandaa kukabiliana na mkono wa sheria.

 

Show More

Related Articles