BiasharaMilele FmSwahili

Serikali yashikilia kuwa hafla ya kuapishwa kwa Raila kama rais itaruhusiwa kuendelea

Serikali imeshikilia msimamo kuwa hafla ya kumwapisha kuwa rais kinara wa NASA Raila Odinga hautaruhusiwa kuendelea. Mkuu wa sheria Githu Muigai ameushutumu muungano huo kwa kupanga njama ya kukiuka sheria na katiba. Muigai ameshikilia kuwa hafla ya kumwapisha rais Kenyatta pekee ndio inayotambulika kisheria na kuwaonya wananasa kukomesha mpango wao anaosema ni sawa na uhaini. Muigai pia amewashutumu baadhi ya wawakilishi wadi katika kaunti mbali mbali kwa kuidhinisha hoja ya kubuni mabunge ya halaiki kinyume cha sheria hasaa baada ya mahakama ya Kitui kuagiza usiitishwe.

Show More

Related Articles