HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakenya Waombwa Kuwa Makini Barabarani

Mwenyekiti wa mamlaka ya Uchukuzi na Usalama barabarani nchini (NTSA), Jackson Waweru amewataka wakenya kuwa makini haswa madereva wasiozingatia kanuni za uendeshaji ili kuepuka  ajali barabarani katika msimu huu wa sherehe na siku zijazo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya  kuhamasisha umma kuhusu usalama barabarani iliyoandaliwa  katika kampuni ya simiti ya Bamburi , Waweru amesema utafiti wao unadhihirisha kuwa asilimia 91 za ajali za barabarani husababishwa na sababu za kibinadamu  huku akiwashuri madereva kutilia maanani usaama kila wanapoendesha magari.

Upande wake, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya simiti ya Bamburi ,Eric Kironde amesema uzinduzi huo utahusisha  msafara kutoka barabara ya Mombasa hadi Malaba kwa siku nne kuhamasisha watu kuhusu usalama wa barabara.

Kironde amewashauri madereva, abiria  na watu wote kwa ujumla kuzingatia kanuni za barabarani na kuwa makini ili kuepuka ajali za barabarani.

 

 

Show More

Related Articles