HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Ruto: Nyongeza ya mshahara ya mtumishi wa umma kutegemea bidii

Wafanyikazi wote kwenye sekta ya umma watalazimika kuongeza bidii katika  utendakazi wao iwapo wanatarajia kupokea nyongeza kwenye mishahara yao pamoja na marupurupu kwenye kipindi hiki kipya cha serikali ya Jubilee.

Naibu Rais William Ruto amesisitiza kuwa japo serikali itatenga kiasi cha shilingi bilioni 85 kwa kipindi cha miaka minne ijayo ili kufanikisha nyongeza hiyo na kuleta usawa kwenye jitihada za kuwatunuku wafanyikazi wake, ni sharti kila mmoja atekeleze wajibu wake kazini ili awe miongoni mwa wale watakaonufaika.

Anders Ihachi alihudhuria kikao cha leo alikohutubia Naibu Rais wakati wa kuwaaga makamishna wanaoondoka wa tume ya kuratibu mishahara na marupurupu, SRC na anatuelezea zaidi.

Show More

Related Articles