HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya kisumu yaondoa kibali cha kuwakamata gavana Outa na Ruth Odinga

Mahakama kuu ya Kisumu imeondopa kibali cha kukamata Seneta Fred Outa na aliyekuwa naibu gavana Ruth Odinga kilichotolewa jana.  Hakimu mkuu Julius Ng’arng’ar ameondoa kibali hicho kufuatia ombi la wakili wa wawili hao Geoffrey yogo ambaye alisema kukosekana kwao mahakamani wakati wa kesi kumetokana na sababu zisizoweza kuepukika. Wawili hao wanakabiliwa na kesi ya kuvuruga vikao vya mafunzo ya maofisa wa IEBC na uharibifu wa mali ya tume hiyo mjini Kisumu mnamo Oktoba 23. Outa anakabiliwa na shtaka lingine la uchochezi wa ghasia. Kesi hizo zitasikilizwa Novemba 28.

Show More

Related Articles