HabariPilipili FmPilipili FM News

Vifo Vya Watoto Vya Pungua Humu Nchini

Vifo vya watoto humu nchini vimepungua kwa asilimia 30 tangu mwaka wa 2008.

Waziri wa fya Cleopa Mailu anasema hii imetokana na kina mama kusaidiwa kujifungua na wakunga walio na ujuzi, watoto kulala ndani ya neti na kuzuia mbu kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaopewa chanjo.

Anasema hii itasaidia kutambua mianya inayohitaji kuzibwa ili kuboresha afya yao, na pia kutambua miradi ambayo inahitaji kufadhiliwa ili kupunguza maambukizi mapya na vifo vya watoto.

Kulingana ni asilimia 60% pekee ya visa vya maradhi ya watoto hasa yale ya homa la mapafu vinavyo ripotiwa hospitani.

Show More

Related Articles