HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Kingorani Kaunti Ya Mombasa Wa Kadiria Hasara Ya Mamilioni Ya Pesa

Mali ya mamilioni ya pesa imeangamia baada ya moto mkubwa kuteketeza nyumba kadhaa eneo la Kingorani eneo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa mapema leo.

Kulingana na Swaleh Abdallah ambae ni miongoni mwa watu ambao nyumba zao zimeteketea katika mkasa huo anasema  moto huo ulianza mwendo wa  saa kumi na mbili asubuhi na kudai kuwa umesababishwa na nyaya za umeme zilizopiga shoti.

Shirika la zima moto wakishirikiana na wakaazi wa eneo hilo wamefanikiwa kuuzima moto huo.

Hata hivyo wakaazi wa eneo hilo wameilaumu kampuni ya kusamabza nguvu za umeme nchini KPLC kwa kutowajibika na kurekebisha magogo ya umeme ambayo ni ya zamani.

 

 

Show More

Related Articles