HabariMilele FmSwahili

Kahiga Mutai kuapishwa leo kama gavana wa Nyeri

Naibu gavana wa Nyeri Kahiga Mutai anatarajiwa kuapishwa leo kuhudumu kama gavana wa kaunti hiyo. Hii ni kufuatia kifo cha aliyekuwa gavana Wahome Gakuru kwenye ajali ya barabarani eneo la Kabati kaunti ya Muranga. Viongozi wa kaunti ya Nyeri wakiongozwa na mbunge Ngunjiri Wambugu wamedhibitisha hafla hiyo itatekelezwa leo kwa mujibu wa sheria. Aidha wanasema uamuzi huu umeungwa mkono na viongozi wote wa Nyeri wakiwemo waakilishi wadi.

Show More

Related Articles