HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Jubilee,IEBC wawasilisha stakabadhi zao dhidi ya kesi ya uchaguzi wa urais

Mahakama ya upeo jumanne hii itakuwa inaanza rasmi mchakato wa kusikiliza kesi nne kuu zinazogusia kura mpya ya urais iliyoandaliwa Oktoba 26 na kumpa Rais Uhuru Kenyatta ushindi kwa mara ya pili kwa kipindi cha miezi miwili unusu hivi baada ya ushindi wake wa kwanza kubatilisha na mahakama mnamo Septemba mosi.

Japo upande wa upinzani NASA baada ya kudai kuwa ulikuwa umejiondoa kwenye marudio ya kura mpya ya urais haukuwasilisha kesi yeyote kibinafsi, utahitajika kujibu kwani umehusishwa kwa njia moja au nyingine kwenye baadhi ya kesi hizo.

Anders Ihachi anaarifu jinsi mtiririko wa mambo utakavyokuwa kuanzia kesho jumatatu ambapo pande zote zinafaa kuwa zimekamilisha kuwasilsha majibu kwa pande kinzani kwenye kesi hizo saa kumi na moja jioni.

Show More

Related Articles