HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta na naibu wakenRuto wahudhuria ibada ya mazishi ya askofu Korir miongoni mwa maelfu ya waumini na viongozi wengine

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto  ni miongoni mwa maelfu ya waumini na waombolezaji wanaohudhuria ibada ya  mazishi ya askofu wa kanisa katoliki Cornelius Korir katika  uwanja wa Eldoret Sports Club. Viongozi wengine  wanaohudhuria ibada hiyo ni pamoja na waziri wa maji Eugene Wamalwa mwenzake wa madini Dan Kazungu magavana Jackson Mandago wa Uasin Gishu , Stephen Sang wa Nandi, Alex Tolgos wa Elgeyo Marakwet. Ni misa inayoongozwa na askofu mkuu wa kanisa katoliki kadinali John Njue  na maaskofu wengine. Ujumbe wa amani umeshamiri kwenye mauhubiri ya leo wakati wa ibada hiyo. Askofu Korir mzaliwa wa kaunti ya Bomet atazikwa kwenye kanisa katoliki la Eldoret kulingana na kanuni za kanisa hilo.

Show More

Related Articles