HabariMilele FmSwahili

Shughli za usafiri kwenye barabara ya Nairobi-Mombasa zakwama kwa zaidi ya saa saba kufuatia ajali ya trela

Shughuli za usafiri kwenye barabara ya Nairobi kuelekea Mombasa zimekwama kwa zaidi ya saa saba kufuatia gari aina ya trela  iliyoanguka  katika soko la salama kaunti ya Makueni. Juhudi za kuondoa trela hiyo ziliambulia patupu baada ya kukwama kwa magari yaliyoletwa kuiondoa. OCPD wa Mukaa Charles Muthui anasema kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari. Anasema walioathirika ni abiria wanaoelekea Makueni Mombasa Machakos na Nairobi. Anasema hali imesababishwa kuwa mbaya zaidi kutokana na mvua iliyonyesha na madereva ambao wamekosa subira.

Show More

Related Articles