HabariMilele FmSwahili

Seneta Mutula asema yapo mapendekezo bungeni ya kubadilisha sheria ya uongozi wa ugavana iwapo aliye mamlakani amefariki ama kujiuzulu

Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior asema yapo mapendekezo katika bunge la seneti kubadilishwa sheria ya kuchukua mamlaka kwa naibu gavana iwapo gavana aliye mamlakani ameaga dunia au amejiuzulu. Seneta huyo anasema mapendekezo hayo yanajumlisha kujadilia majukumu ya manaibu wa gavana nchini ili wasiendelee kuwa mamlakani bila kuwajibikia lolote. Mapendekezo haya yamechangiwa pakubwa na kifo cha gavana wa Nyeri Wahome Gakuru, ambacho kimezua pengo la uongozi, hivyo kuhitaji kutatuliwa kwani sheria ya sasa imevutia mseto hisia.

Show More

Related Articles